1 Kut 20:4,5;Law 19:4;Kum 4:16-19;5:8;16:21-22;27:1;Isa 44:9-20;Zab 97:7 Msifanye sanamu yoyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 2 Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.
3 Kum 11:13-15;28:1-14 Mkizifuata amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya; 4 Kum 28:12;Isa 30:23 ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa mavuno yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Kum 11:15;Yoe 2:19,26;Ayu 11:18;Eze 34:25 Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuishi katika nchi yenu salama. 6 1 Nya 22:9;Isa 45:7;Zab 3:5;Yer 30:10;Yn 14:27;Rum 5:1;2 Fal 17:25;Eze 5:17;14:15,17;Yos 23:10 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala na hakuna atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu. 7 Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga. 8 Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia moja, na watu mia moja wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga. 9 Kut 2:25;2 Fal 13:23;Mwa 17:6,7 Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi. 10 Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya. 11 Eze 37:26;Kum 32:19 Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia. 12 2 Kor 6:16;Efe 2:21;Ebr 3:6;Eze 11:20 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 13 Eze 34:27 Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawafanya mwende sawasawa.
14 Kum 28:15 Lakini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote; 15 2 Fal 17:15 nanyi mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia amri zangu, hata ikawa hamtaki kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu; 16 Kum 28:22;1 Sam 2:33;Ayu 31:8 mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila. 17 Amu 2:14;Zab 106:41;53:5 Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.
18 1 Sam 2:5 Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 19 1 Sam 4:10;Isa 25:11 Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba; 20 Zab 127:1;Isa 49:4;Kum 28:18;Hag 1:10 na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake. 21 Nanyi ikiwa mnaenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo. 22 Kum 32:24;2 Fal 17:25;Yer 15:3;Amu 5:6;2 Nya 15:5;Zek 7:14 Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang’anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa. 23 Yer 5:3 Tena kama hamtaki kurejeshwa upya kwangu mimi kwa mambo haya, bali mnaendelea kunifanyia kinyume; ndipo nami nitaendelea kuwafanyia kinyume; 24 2 Sam 22:27 nami nitawapiga, mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 25 Eze 6:3;Kum 28:22;Hes 14:12;16:49;Amo 4:10 Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mikononi mwa adui. 26 Isa 3:1;Mik 6:14 Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuri moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba.
27 Tena ikiwa baada ya hayo yote hamtaki kunisikiza, bali mnaenda kinyume; 28 Isa 59:18 ndipo nami nitawaendea kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu. 29 2 Fal 6:29 Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila. 30 2 Nya 34:3;2 Fal 23:20;Zab 78:59 Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia. 31 Neh 2:3;Yer 5:10;22:5;Zab 74:1-8;Yer 26:6,9;Omb 1:10;Eze 9:6 Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo. 32 Yer 9:11;25:11 Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia. 33 Kum 4:27;28:64;Zab 44:11;Eze 12:15;20:23;Zek 7:14 Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo. 34 Law 25:2-4;2 Nya 36:21 Hapo ndipo nchi itakapozifurahia Sabato zake, wakati itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake. 35 Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo mapumziko ambayo haikuwa nayo katika Sabato zenu, hapo mlipokaa katika nchi hiyo. 36 Mwa 35:5;Yos 2:9-11;Eze 21:7;Mit 28:1 Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye. 37 Amu 7:22;Isa 10:4;Amu 2:14 Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu. 38 Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza. 39 Neh 1:9;Yer 3:25;20:12 Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao. 40 Hes 5:7;1 Fal 8:33;Ayu 34:31;Mit 28:13;Yer 3:12;Lk 15:18;1 Yoh 1:9 Nao wataukiri uovu wao, na uovu wa baba zao, katika maasi yao waliyoasi juu yangu, tena kwa kuwa wameendelea kunifanyia kinyume, 41 Yer 9:25;Eze 44:7;Mdo 7:51;Rum 2:29;Kol 2:11;1 Fal 21:29;2 Nya 12:6 mimi nami nimewaendea kinyume, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao; 42 Mwa 17:7-8;26:3-4;28:13-14;Kut 2:24;6:5;Zab 106:5;Eze 16:60;Zab 136:23 ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo. 43 Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu. 44 Kum 4:31 Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao; 45 Rum 11:28;Eze 20:9 lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi BWANA.
46 Kum 33:4;Yn 1:17 Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.