Yesu ahubiri katika Galilaya
35 Lk 4:42-44Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. 36 Simoni na wenziwe wakamfuata; 37 nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. 38 Akawaambia, Twendeni mahali pengine, katika vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana nilikuja kwa ajili ya hilo. 39 Mt 4:23;9:35Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.