35 Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, 37 nao walipomwona, wakapaza sauti, wakasema, "Kila mtu anakutafuta!"
38 Isa akawajibu, "Twendeni mahali pengine, kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia. Maana nilikuja kwa kusudi hili." 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.
Isa amtakasa mtu mwenye ukoma
(Mathayo 8:1-4; Luka 5:12-16)