Kuharibiwa kwa hekalu
1 Mt 24:1-51;Lk 21:5-36Alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya! 2 Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitabaki hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.
3 Na alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha, 4 Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?