Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 13:1-4

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Kubomolewa kwa Hekalu kwatabiriwa

1 Isa alipokuwa akitoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, "Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!"

2 Ndipo Isa akajibu akasema, "Je, unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali yote yatabomolewa."

Ishara za nyakati za mwisho

(Mathayo 24:3-14; Luka 21:7-19)

3 Isa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni mkabala na Hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamuuliza faraghani, 4 "Tafadhali tuambie, mambo haya yatatukia lini? Nayo dalili ya kuwa hayo yote yanakaribia kutimia itakuwa gani?"

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mt 24:1-51;Lk 21:5-36Alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya! 2 Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitabaki hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

    3 Na alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha, 4 Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Yesu alipokuwa akitoka Hekaluni, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, "Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!"

    2 Ndipo Yesu akajibu akasema, "Je, unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali yote yatabomolewa."

    3 Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni mkabala na Hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamuuliza faraghani, 4 "Tafadhali tuambie, mambo haya yatatukia lini? Nayo dalili ya kuwa hayo yote yanakaribia kutimia itakuwa gani?"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.