Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 3

Mtu mwenye mkono uliopooza

1 Mt 12:9-14;Lk 6:6-11Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. 5 Yn 11:33Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

Veja também