Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 4

3 Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda; 4 ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. 5 Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na udongo haba; 6 hata jua lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina mizizi ikanyauka. 7 Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda. 8 Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia. 9 Akasema, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também