Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 6

Kuwalisha watu elfu tano

30 Lk 9:10;10:17Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha. 31 Akawaambia, Njooni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 32 Mt 14:13-21;Lk 9:11-17;Yn 6:1-13Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu. 33 Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika. 34 Hes 27:17;1 Fal 22:17;2 Nya 18:16;Eze 34:5;Mt 9:36Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35 Mk 8:1-9Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36 uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. 37 Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari6:37 Dinari moja ni ujira wa kazi ya kutwa. mia mbili ili tuwape kula? 38 Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. 39 Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. 40 Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. 41 Mk 7:34Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 42 Wakala wote wakashiba. 43 Kum 28:5Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. 44 Na walioila ile mikate walikuwa wanaume elfu tano.

Veja também