Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 7

9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 10 Kut 20:12;21:17;Law 20:9;Kum 5:16Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. 11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokezana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Veja também