Kuwalisha watu elfu nne
1 Mt 15:32-39Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, 2 Mk 6:34-44Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; 3 nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao wakiwa na njaa, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. 4 Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? 5 Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, 6 Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; wakawaandalia mkutano. 7 Walikuwa na visamaki vichache; akavibariki, akasema wawagawie na hivyo pia. 8 Kum 28:5Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate vikapu saba. 9 Na watu waliokula walikuwa elfu nne. Akawaaga.