Yesu amsifu Yohana Mbatizaji
7 Mt 3:1,5Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 8 Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. 9 Lk 1:76Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. 10 Mal 3:1;Mk 1:2;Yn 3:28Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,
Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu
Mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.