Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 13

13 Kum 29:4Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. 14 Isa 6:9-10;Yn 12:40;Mdo 28:26,27Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,

Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;

Kutazama mtatazama, wala hamtaona.

15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,

Na kwa masikio yao hawasikii vema,

Na macho yao wameyafumba;

Wasije wakaona kwa macho yao,

Wakasikia kwa masikio yao,

Wakaelewa kwa mioyo yao,

Wakaongoka, nikawaponya.

Veja também