Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 16

Chachu ya Mafarisayo na Masadukayo

5 Nao wanafunzi wakaenda hadi ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate. 6 Lk 12:1Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8 Mt 6:30Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamna mikate? 9 Mt 14:17-21Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota? 10 Mt 15:34-38Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota? 11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa sikuwaambia kwa sababu ya mkate? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 12 Yn 6:27Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Veja também