Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 17:9-13

SRUV Swahili Revised Union Version

9 Mt 16:20Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu yeyote habari ya maono hayo, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. 10 Mal 4:5;Mt 11:14Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12 Mt 11:14;14:9,10ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. 13 Lk 1:17Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawaagiza, "Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu."

    10 Wale wanafunzi wakamuuliza, "Kwa nini basi walimu wa Torati husema kwamba ni lazima Ilya aje kwanza?"

    11 Isa akawajibu, "Ni kweli, Ilya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. 12 Lakini nawaambia, Ilya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao." 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yahya.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaagiza, "Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu."

    10 Wale wanafunzi wakamuuliza, "Kwa nini basi walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?"

    11 Yesu akawajibu, "Ni kweli, Eliya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. 12 Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao." 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yohana Mbatizaji.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.