9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawaagiza, "Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu."
10 Wale wanafunzi wakamuuliza, "Kwa nini basi walimu wa Torati husema kwamba ni lazima Ilya aje kwanza?"
11 Isa akawajibu, "Ni kweli, Ilya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. 12 Lakini nawaambia, Ilya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao." 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yahya.
Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu
(Marko 9:14-29; Luka 9:37-45)