Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 20

Yesu aponya vipofu wawili

29 Mk 10:46-52;Lk 18:35-43Walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata. 30 Mt 15:22Na tazama, vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! 31 Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! 32 Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini? 33 Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe. 34 Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.

Veja também