31 Lk 18:14Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa kwanza. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. 32 Lk 3:12;7:29-30Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Mathayo 21:31,32
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
31 "Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?"
Wakamjibu, "Ni yule wa kwanza."
Isa akawaambia, "Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika ufalme wa Mungu. 32 Kwa maana Yahya alikuja kwenu kuwaonesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
31 "Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?"
Wakamjibu, "Ni yule wa kwanza."
Yesu akawaambia, "Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu. 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.