31 "Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?"
Wakamjibu, "Ni yule wa kwanza."
Isa akawaambia, "Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika ufalme wa Mungu. 32 Kwa maana Yahya alikuja kwenu kuwaonesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.
Mfano wa wapangaji waovu
(Marko 12:1-12; Luka 20:9-19)