Mfano wa talanta
14 Lk 19:11-27Maana itakuwa kama mfano wa mtu aliyetaka kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.Mt 21:3315 Rum 12:6Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. 17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. 18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. 20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21 Mt 25:23;Mt 24:45-47;Lk 16:10Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23 Mt 25:21Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nilitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29 Mt 13:12;Mk 4:25;Lk 8:18Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. 30 Mt 8:12;22:13;Lk 13:28Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.