Kuzikwa kwa Yesu
57 Mk 15:42-47;Lk 23:50-55;Yn 19:38-42Na ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;Kut 34:2558 mtu huyu alimwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe. 59 Yusufu akautwaa mwili, akauzongazonga katika sanda ya kitani safi, 60 Isa 53:9akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.