57 Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Isa. 58 Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Isa. Pilato akaamuru apewe. 59 Yusufu akauchukua mwili wa Isa, akaufunga kwa kitambaa cha kitani safi, 60 na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.
Mathayo 27:57-60
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
57 Mk 15:42-47;Lk 23:50-55;Yn 19:38-42Na ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;Kut 34:2558 mtu huyu alimwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe. 59 Yusufu akautwaa mwili, akauzongazonga katika sanda ya kitani safi, 60 Isa 53:9akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
57 Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59 Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, 60 na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.