2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. 3 Mt 17:2;Mdo 1:10Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. 4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.