5 Mt 27:53Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 Zab 91:11-12akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake;
Na mikononi mwao watakuchukua;
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Kum 6:16Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.