Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 4:5-7

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

5 Ndipo ibilisi akampeleka Isa hadi mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu4:5 Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu., 6 akamwambia, "Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa:

" ‘Atakuagizia malaika wake,

nao watakuchukua mikononi mwao

ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ "

7 Isa akamjibu, "Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’ "

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Mt 27:53Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 Zab 91:11-12akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa,

    Atakuagizia malaika zake;

    Na mikononi mwao watakuchukua;

    Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

    7 Kum 6:16Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, 6 akamwambia, "Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa:

    " ‘Atakuagizia malaika zake,

    nao watakuchukua mikononi mwao

    ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ "

    7 Yesu akamjibu, "Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ "

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.