Kuhusu hazina
19 Yak 5:2-3Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba; 20 Mt 19:21;Lk 12:33,34;Kol 3:1,2bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako pia.
Kutumikia mabwana wawili
24 Lk 16:9,13Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
33 Rum 14:17;1 Fal 3:13,14;Zab 37:4,25Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.