Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 9

Msichana arejeshewa uhai na mwanamke kuponywa

18 Mk 5:22-43;Lk 8:41-56Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja kiongozi mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. 19 Yesu Akaondoka, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.

20 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. 21 Mt 14:36Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. 22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, 24 Yn 11:11,14,25akawaambia, Ondokeni; kwa maana msichana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. 25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule msichana akasimama. 26 Habari hizi zikaenea katika nchi ile yote.

Veja também