Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 9

Yesu amponya mtu aliyepooza

2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, akiwa amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 3 Mk 2:7Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. 4 Mt 12:25;Yn 2:25Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? 6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Inuka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. 7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.

Veja também