Ezra atoa mwito wa kutii sheria
1 Neh 3:26;12:37;Ezr 7:6;Isa 8:20;Yer 8:8,9;2 Nya 34:15;Mal 4:4Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha Torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli. 2 Kum 31:11,12;1 Pet 3:7;Law 23:24Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba. 3 Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati. 8 Hab 2:2;Mdo 8:30-35Nao wakasoma katika kitabu, katika Torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa.
9 Ezr 2:63;Neh 7:65;2 Nya 35:3;Hos 4:6;Law 23:24;Kum 16:14;Mhu 3:4;Mal 2:13Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha,8:9 Tazama Neh 7:65,70. na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.