1 watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja kwenye uwanja mbele ya Lango la Maji. Wakamwambia Ezra mwandishi alete Kitabu cha Torati ya Musa, ambacho Mwenyezi Mungu aliamuru kwa ajili ya Israeli.
2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Torati mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu. 3 Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko hadi adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Torati.
8 Walisoma kutoka kile Kitabu cha Torati ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.
9 Ndipo Nehemia aliyekuwa mtawala8:9 au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi., Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, "Siku hii ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Msiomboleze wala msilie." Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Torati.