10 2 Kor 5:10;Mdo 17:31;Mt 25:31,32Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11 Isa 45:23;49:18;Flp 2:10,11Kwa kuwa imeandikwa,
Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu;
Na kila ulimi utamkiri Mungu.
12 Gal 6:5Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.