16 Naye Ruthu akasema,
Usinisihi nikuache,
Nirudi nisifuatane nawe;
Maana wewe uendako nitakwenda,
Na wewe ukaapo nitakaa.
Watu wako watakuwa watu wangu,
Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17 1 Sam 3:17;25:25;2 Fal 6:31Pale utakapofia ndipo nitakufa nami,
Na papo hapo nitazikwa;
BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi,
Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.