Admiração
O temor do Senhor é o princípio da sabedoria. A admiração reverente por Deus é a postura que produz conhecimento, obediência e bênção na vida do crente.
Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
"Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Kumcha Mwenyezi Mungu humfundisha mtu hekima,
nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.
Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu,
kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
Kumcha Mwenyezi Mungu ni kuchukia uovu;
ninachukia kiburi na majivuno,
tabia mbaya na mazungumzo potovu.
Unyenyekevu na kumcha Mwenyezi Mungu
huleta utajiri, heshima na uzima.
Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;
mche Mwenyezi Mungu ukajiepushe na uovu.
Hii itakuletea afya mwilini mwako,
na lishe kwenye mifupa yako.
Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu,
na uzuri unapita upesi;
bali mwanamke anayemcha Mwenyezi Mungu atasifiwa.
Hii ndiyo jumla ya maneno;
yote yamekwisha sikiwa:
Mche Mungu, nawe uzishike amri zake,
maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.
Baraka za mwenye haki
Msifuni Mwenyezi Mungu.
Heri mtu yule amchaye Mwenyezi Mungu,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu
Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,
wanaoenda katika njia zake.
Lakini macho ya Mwenyezi Mungu yako kwa wale wamchao,
kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
Mungu atatubariki
na miisho yote ya dunia itamcha yeye.
Bali ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.
Mche Mwenyezi Mungu
Na sasa, ee Israeli, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, anataka nini kwako ila kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kuyashika maagizo ya Mwenyezi Mungu na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?
Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.
Wapendwa, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.
Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.
"Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,
hata akiacha uchaji wa Mwenyezi.