Publicidade

Admiração

Por Bíblia Online

O temor do Senhor é o princípio da sabedoria. A admiração reverente por Deus é a postura que produz conhecimento, obediência e bênção na vida do crente.

Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;

Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima;

Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA;

Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.

Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;

Kiburi na majivuno, na njia mbovu,

Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA

Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.

Usiwe na hekima machoni pako;

Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.

Itakuwa afya mwilini pako,

Na mafuta mifupani mwako.

Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;

Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.

Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;

Mche Mungu, nawe uzishike amri zake,

Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,

Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri,

Sifa zake zadumu milele.

Baraka za mwenye haki

Haleluya.

Heri mtu yule amchaye BWANA,

Apendezwaye sana na maagizo yake.

Nyumba ya mwumini yenye furaha

Heri kila mtu amchaye BWANA,

Aendaye katika njia yake.

Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,

Wazingojeao fadhili zake.

Mungu atatubariki sisi;

Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.

Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.

Umuhimu wa kuwa na amri

Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzifuata amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?

Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

Ilikuwa kwa sababu wale wakunga walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.

Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu kutoka kwa uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.

Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki;

Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-