Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 67

Mataifa yaitwa kumsifu Mungu

Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.

1 Zab 4:6;31:16;119:135;Hes 6:25,26;2 Kor 4:6 Mungu na atufadhili na kutubariki,

Na kutuangazia uso wake.

2 Mdo 13:10;Tit 2:11;Lk 2:30-32 Njia yake ijulikane duniani,

Wokovu wake katikati ya mataifa yote.

3 Isa 24:15,16 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,

Watu wote na wakushukuru.

4 Zab 96:10 Mataifa na washangilie,

Naam, waimbe kwa furaha,

Maana kwa haki utawahukumu watu,

Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.

5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,

Watu wote na wakushukuru.

6 Law 26:4;Isa 1:19;Zab 85:9-12 Nchi imetoa mazao yake

MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.

7 Zab 22:27 Mungu atatubariki sisi;

Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.

Veja também