Agradecimento pela família
Agradecer pela família é reconhecer a bênção mais preciosa que Deus nos concede. Os filhos são herança do Senhor — cada membro da família é presente divino a ser celebrado.
Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,
uzao ni zawadi kutoka kwake.
Kama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
Heri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.
Upendo wa Mwenyezi Mungu
Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu.
Vyote vilivyo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu,
wala usisahau wema wake wote:
Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Mwenyezi Mungu,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.
Wana wa wana ni taji la wazee,
nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
Niliomba mtoto huyu, naye Mwenyezi Mungu amenijalia kile nilichomwomba.
Shukrani na maombi
Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.
Je, tutawezaje kumshukuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu?
Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi jamaa za mataifa,
mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu,
Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.
Wanawake wakamwambia Naomi: "Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, asiyekuacha bila kuwa na jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe mashuhuri katika Israeli yote! Atakurejeshea uhai wako na kukuangalia katika siku za uzee wako. Kwa maana mkweo ambaye anakupenda, na ambaye kwako ni bora zaidi ya watoto wa kiume saba, ndiye alimzaa."
Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,
kama ninavyofanya leo.
Baba huwaambia watoto wao
habari za uaminifu wako.