Publicidade

Ajuda

Por Bíblia Online

Deus é nosso auxílio e socorro em todo tempo. Ele não dorme nem cochila. O Senhor é nosso ajudador — não precisamos temer o que o homem possa nos fazer.

Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Hakika Mungu ni msaada wangu,

Bwana ndiye anayenitegemeza.

Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

yeye ni ngome yao wakati wa shida.

Mwenyezi Mungu huwasaidia na kuwaokoa,

huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,

kwa maana wanamkimbilia.

Ee Bwana Mwokozi wangu,

uje upesi kunisaidia.

Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,

kwa ajili ya utukufu wa jina lako;

tuokoe na kutusamehe dhambi zetu

kwa ajili ya jina lako.

Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,

kwa maana amesikia kilio changu

nikimwomba anihurumie.

Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

Kama Mwenyezi Mungu hangenisaidia upesi,

ningeishi katika kimya cha kifo.

Kwa maana Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

Hufanya msaada wa wokovu wako kuwa ngao yangu;

msaada wako umeniinua niwe mkuu.

Isa awaita waliolemewa na mizigo

"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.

Vivyo hivyo, Roho wa Mungu hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa. Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huyo huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu.

Mtumaini Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-