Publicidade

Ajuda

Por Bíblia Online

Deus é nosso auxílio e socorro em todo tempo. Ele não dorme nem cochila. O Senhor é nosso ajudador — não precisamos temer o que o homem possa nos fazer.

Msaada wangu hutoka kwa BWANA,

Aliyezifanya mbingu na nchi.

Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;

Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.

Na wokovu wa wenye haki una BWANA;

Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.

Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa;

Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya;

Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

Ufanye haraka kunisaidia,

Ee Bwana, wokovu wangu.

Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,

Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.

Utuokoe, utusamehe dhambi zetu,

Kwa ajili ya jina lako.

Na ahimidiwe BWANA.

Maana ameisikia sauti ya dua yangu;

BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.

Moyo wangu umemtumaini,

Nami nimesaidiwa;

Basi, moyo wangu unashangilia,

Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,

Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.

Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.

Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;

Na unyenyekevu wako umenikuza.

Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Katika njia zako zote mkiri yeye,

Naye atayanyosha mapito yako.

huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-