Publicidade

Salmos 94

Mungu amlipiziaye mwenye haki

1 Ee BWANA, Mungu wa kisasi,

Mungu wa kisasi, uangaze,

2 Mwa 18:25 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze,

Uwape wenye kiburi stahili zao.

3 Ayu 20:5 BWANA, hadi lini wasio haki,

Hadi lini wasio haki watashangilia?

4 Yud 1:15 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno,

Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?

5 Ee BWANA, wanawaponda watu wako;

Wanautesa urithi wako;

6 Wanamwua mjane na mgeni;

Wanawaua yatima.

7 Nao husema, BWANA haoni;

Mungu wa Yakobo hatambui.

8 Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini;

Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?

9 Kut 4:11;Mit 20:12 Aliyelitia sikio mahali pake, asisikie?

Aliyelifanya jicho, asione?

10 Ayu 35:11;Yn 6:45;Isa 2:3;28:26 Awaadibuye mataifa, asikemee?

Amfundishaye mwanadamu, asijue?

11 1 Kor 1:21;3:20 BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,

Ya kuwa ni ubatili.

12 Ayu 5:17;Mit 3:11;1 Kor 11:32 Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye,

Na kumfundisha kwa sheria yako;

13 Ukimponya katika siku za shida,

Hadi asiye haki atakapochimbiwa shimo.

14 Kum 31:6;1 Sam 12:22;1 Fal 6:13;Yer 31:37 Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,

Wala hutauacha urithi wake,

15 Maana hukumu itarejea kwa wenye haki,

Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.

16 Ni nani atakayesimama

Kwa ajili yangu juu ya wabaya?

Ni nani atakayenisaidia

Juu yao wafanyao maovu?

17 Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,

Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.

18 Niliposema, Mguu wangu unateleza;

Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.

19 Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu,

Faraja zako zinaifurahisha roho yangu.

20 Amo 6:3;2 Kor 6:14;Zab 58:2;Isa 10:1 Je! Watawala waovu wanaweza kushirikiana nawe,

Wale watungao madhara kwa njia ya sheria?

21 Mt 27:1;Kut 23:7;Mit 17:15 Kwa pamoja wanaishambulia nafsi yake mwenye haki,

Na kuihukumu damu isiyo na hatia.

22 Lakini BWANA amekuwa ngome kwangu,

Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.

23 Mit 2:22 Naye atawarudishia uovu wao,

Atawaangamiza katika ubaya wao,

Naam, BWANA, Mungu wetu, atawaangamiza.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-