Aliança
A aliança é o modo como Deus se relaciona com seu povo. Da aliança com Noé à Nova Aliança em Cristo, Deus se compromete com amor e fidelidade irrevogáveis.
Alianças com Israel
Deus firmou aliança com Abraão, Moisés e Davi. No arco-íris, na lei, nas promessas — Ele é o Deus da aliança.
Ndipo Mungu akamwambia Nuhu na wanawe pamoja naye: "Sasa mimi ninaweka agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: ndege, mifugo, na wanyama pori wote, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi: kila kiumbe hai duniani. Ninaweka agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika; kamwe hakutakuwa tena gharika ya kuangamiza dunia."
Mungu akasema, "Hii ni ishara ya agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, agano kwa vizazi vyote vijavyo: Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia.
Ninaweka agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika; kamwe hakutakuwa tena gharika ya kuangamiza dunia."
Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia.
Siku hiyo Mwenyezi Mungu akafanya agano na Abramu, na kumwambia, "Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri hadi mto ule mkubwa, Frati: yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Wahiti, Waperizi, Warefai, Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi."
Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, "Kwangu mimi, hili ndilo agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. Hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Ibrahimu, kwa maana nimekufanya baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana; kwako yatatoka mataifa, na wafalme watatoka kwako. Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo, nami nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako. Nchi yote ya Kanaani, unayoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na ya uzao wako; nami nitakuwa Mungu wao."
Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu, "Kwako wewe, lazima ushike agano langu, wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo. Hili ni agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa, na hii itakuwa ni alama ya agano kati yangu na ninyi.
Mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walienda vitani na wakawashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,
Sasa, mkinitii kikamilifu na kutunza agano langu, basi ninyi mtakuwa hazina yangu ya pekee miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu,
"Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao.
Kisha Mwenyezi Mungu akasema: "Tazama, ninafanya agano nanyi. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza kazi nitakayowafanyia Mimi, Mwenyezi Mungu wenu.
Musa alikuwa huko pamoja na Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya agano, yaani zile Amri Kumi.
Musa alikuwa huko pamoja na Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya agano, yaani zile Amri Kumi.
Aliwatangazia agano lake, hizo Amri Kumi ambazo aliwaamuru mzifuate, kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe.
Basi ujue kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake.
Alianças renovadas
O povo renovava a aliança diante do Senhor. A fidelidade de Deus permanece mesmo quando o povo falha.
Basi, watu walipovunja kambi ili kuvuka Yordani, makuhani wakiwa wamebeba Sanduku la Agano waliwatangulia. Wakati huu ulikuwa wakati wa mavuno, nao Mto Yordani ulikuwa umefurika hadi kwenye kingo zake. Ilikuwa kawaida ya Yordani kufurika nyakati zote za mavuno. Mara tu makuhani wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Agano walipofika mtoni na nyayo zao kuzama ndani ya yale maji, maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.
Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Mto Yordani, wakati Waisraeli wote wakiwa wanapita hadi taifa lote likaisha kuvuka mahali pakavu.
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi Mungu. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu.
Mfalme akasimama karibu na nguzo, na kufanya upya agano mbele za Mwenyezi Mungu: kwamba atamfuata Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake, maagizo na sheria zake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, na hivyo kuyathibitisha maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika agano.
Kwa hiyo wakati ule Mfalme Yehoramu akaondoka kutoka Samaria na kukusanya Israeli yote tayari kwenda vitani. Akapeleka pia ujumbe ufuatao kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda: "Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je, utaenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?"
Akajibu, "Nitaenda pamoja nawe. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako."
Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: "Mwenyezi Mungu na awaangamize adui za Daudi." Naye Yonathani akamtaka Daudi athibitishe tena kiapo chake cha kumpenda, kwa sababu Yonathani alimpenda Daudi kama nafsi yake mwenyewe.
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Haruni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza. Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya agano langu la amani naye. Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli."
Musa alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na Mwenyezi Mungu, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Musa akazungumza na Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Sema na Waisraeli, na ujipatie fimbo kumi na mbili kutoka kwao, moja kutoka kwa kila mmoja wa viongozi wa makabila ya baba zao. Andika jina la kila mtu kwenye fimbo yake. Kwenye fimbo ya Lawi andika jina la Haruni, kwa maana ni lazima iwepo fimbo moja kwa kila kiongozi kwa ajili ya kila kabila la baba zao. Ziweke hizo fimbo ndani ya Hema la Kukutania mbele ya Sanduku la Ushuhuda, mahali nikutanapo nawe. Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manung’uniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako."
Hivyo Musa akasema na Waisraeli, nao viongozi wao wakampa fimbo kumi na mbili, fimbo moja kwa ajili ya kila kabila la baba zao, nayo fimbo ya Haruni ikiwa miongoni mwa hizo. Musa akaziweka hizo fimbo mbele za Mwenyezi Mungu ndani ya Hema la Ushuhuda.
Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Haruni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi. Ndipo Musa akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele za Mwenyezi Mungu. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Rudisha fimbo ya Haruni mbele ya Sanduku la Ushuhuda, ili ihifadhiwe kama alama kwa waasi. Hili litakomesha manung’uniko yao dhidi yangu, ili wasife." Musa akafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru.
Waisraeli wakafanya maovu mbele za Mwenyezi Mungu tena; na kwa kuwa walifanya maovu hayo, Mwenyezi Mungu akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli. Egloni akawakusanya Waamoni na Waamaleki kwake, wakashambulia Israeli, na wakatwaa Mji wa Mitende.
Nova Aliança
Eis que dias vêm em que farei nova aliança. Jesus é mediador de uma aliança superior, fundamentada em melhores promessas.
"Siku zinakuja," asema Mwenyezi Mungu,
"nitakapofanya agano jipya
na nyumba ya Israeli
na nyumba ya Yuda.
Halitafanana na agano
nililofanya na baba zao
wakati nilipowashika mkono
kuwaongoza watoke Misri,
kwa sababu walivunja agano langu,
ijapokuwa nilikuwa mume kwao,"
asema Mwenyezi Mungu.
"Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile," asema Mwenyezi Mungu.
"Nitaweka sheria yangu katika nia zao,
na kuiandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
Mtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema,
‘Mjue Mwenyezi Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,"
asema Mwenyezi Mungu.
"Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena."
"Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala kwenye kiti chake cha utawala.
Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.
Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.
Lakini huduma aliyopewa Isa ni bora kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi ya lile la zamani, nalo limewekwa misingi ya ahadi zilizo bora zaidi.
Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Isa, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni pake, kupitia kwa Isa Al-Masihi, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.
Ndiye alitutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho wa Mungu; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima.
Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, linalozaa watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hajiri. Basi Hajiri anawakilisha Mlima Sinai ulio Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu.
Fidelidade da aliança
A aliança de Deus é eterna. Ele não quebra seu pacto nem altera o que saiu dos seus lábios.
Lakini kutoka milele hata milele
upendo wa Mwenyezi Mungu uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
kwa wale walishikao agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.
"Bali mimi, hili ndilo agano langu nao," asema Mwenyezi Mungu. "Roho wangu Mtakatifu, aliye juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka vinywani vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele," asema Mwenyezi Mungu.
" ‘Nitafanya nao agano la amani na kuwaondoa wanyama mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama.
Mwenyezi Mungu mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."
Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu, atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu."
"Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi yake, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi. Baada ya miaka kadhaa, wataungana. Binti ya mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini nguvu za huyo binti hazitadumu; hata mfalme hatadumu wala nguvu zake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, na baba yake, na yeyote aliyemuunga mkono.
Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza. Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote, na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia.
"Nimefanya agano na macho yangu
yasimtazame msichana kwa kumtamani.
Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,
kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno
ya kushawishi kutenda ubaya,
aliyemwacha mwenzi wa ujana wake
na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.