Publicidade

Bem

Por Bíblia Online

Fazer o bem é mandamento de Deus e expressão prática do amor cristão. A Bíblia convida a praticar o bem a todos, com alegria, sem se cansar — porque colheremos no tempo próprio.

Aache uovu, atende mema,

aitafute amani na kuifuatilia.

Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema.

Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

Nami bado nina tumaini hili:

nitauona wema wa Mwenyezi Mungu

katika nchi ya walio hai.

Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, rehema zako kuu na upendo,

kwa maana zimekuwepo tangu zamani.

Usizikumbuke dhambi za ujana wangu

wala njia zangu za uasi,

sawasawa na upendo wako unikumbuke,

kwa maana wewe ni mwema, Ee Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu ni mwenye haki katika njia zake zote,

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki,

na sawa: yaani kila njia nzuri.

Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,

afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

Lakini tunda la Roho wa Mungu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waumini.

Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yanayofaa kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.

Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.

Alama za Mfuasi wa kweli wa Al-Masihi

Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Fanyeni yote kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu

"Vitu vyote ni halali," lakini si vitu vyote vilivyo na faida. "Vitu vyote ni halali," lakini si vyote vinavyojenga.

Msidanganyike: "Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema."

Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.

Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.

Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani wale walio na juhudi katika kutenda mema.

Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa; katika utauwa, upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu, upendo.

Kuvumilia mateso

Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema?

Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu:

"Simama kwenye njia panda utazame,

ulizia mapito ya zamani,

ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,

nanyi mtapata amani nafsini mwenu.

Lakini ninyi mlisema, Hatutaipita njia hiyo.

Mwenyezi Mungu ni Mwema,

kimbilio wakati wa taabu.

Huwatunza wale wanaomtegemea,

Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliye ndani ya ile nyumba. Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-