Casa de Deus
A casa de Deus é lugar de adoração, refúgio e encontro com o Sagrado. A Bíblia exalta o tabernáculo, o templo e a igreja como morada do Altíssimo entre seu povo.
A presença de Deus
Quão amáveis são os teus tabernáculos! Uma coisa pedi ao Senhor: habitar na casa do Senhor todos os dias da minha vida.
Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu kwingineko;
Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu,
Kuliko kuishi katika hema za uovu.
Neno moja nimelitaka kwa BWANA,
Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa BWANA
Siku zote za maisha yangu,
Niutazame uzuri wa BWANA,
Na kutafakari hekaluni mwake.
Heri mtu yule umchaguaye,
Na kumkaribisha akae nyuani mwako.
Na tushibe wema wa nyumba yako,
Patakatifu pa hekalu lako.
Nilifurahi waliponiambia,
Twende nyumbani kwa BWANA.
Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Bali mimi ni kama mzeituni
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
Maana mvuto wa nyumba yako umenila,
Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
O templo
Minha casa será chamada casa de oração. O zelo da tua casa me consumiu. O verdadeiro templo é o corpo do cristão.
Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Akasokota kikoto cha kamba, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.
Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye kulingana na mfano ule aliouona; ambayo baba zetu, kwa kupokezana, wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki ya Mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi; aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. Lakini Sulemani alimjengea nyumba. Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,
Mbingu ni kiti changu cha enzi,
Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu;
Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana,
Au ni mahali gani nitakapostarehe?
Si mkono wangu uliofanya haya yote?
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, ijapokuwa mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.