Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yungiyungi. Ya Daudi.
1 Ee Mungu, uniokoe,
Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
2 Ninazama katika matope mengi,
Pasipowezekana kusimama.
Nimefika penye maji ya vilindi,
Mkondo wa maji unanigharikisha.
3 Nimechoka kwa kulia kwangu,
Koo yangu imekauka.
Macho yangu yamedhoofika
Kwa kumngoja Mungu wangu.
4 Zab 35:19;Yn 15:25 Wanaonichukia bure ni wengi
Kuliko nywele za kichwa changu.
Watakao kunikatilia mbali ni wengi,
Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.
Hata mimi nililipishwa kwa nguvu
Vitu nisivyovichukua.
5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu,
Wala hukufichwa dhambi yangu.
6 Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe,
Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi.
Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe,
Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu,
Fedheha imenifunika uso wangu.
8 Isa 53:3;Yn 1:11 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,
Na asiyetambuliwa na wana wa mama yangu.
9 1 Fal 19:10;Zab 119:139;Yn 2:17;Rum 15:3 Maana mvuto wa nyumba yako umenila,
Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga,
Nikalaumiwa kwa hayo.
11 1 Fal 9:7;Yer 24:9;Zab 44:13,14 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu,
Nikawa kifani cha dharau kwao.
12 Ayu 17:6;Omb 3:14 Waketio langoni hunisema,
Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
13 Isa 49:8;2 Kor 6:2 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA,
Wakati ukupendezao; Ee Mungu,
Kwa wingi wa fadhili zako unijibu,
Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni,
Wala usiniache nikazama.
Na niponywe kutoka kwa wanaonichukia,
Na kutoka katika vilindi vya maji.
15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze,
Wala Shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
16 Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema,
Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.
17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako,
Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
18 Uikaribie nafsi yangu, uikomboe,
Kwa sababu ya adui zangu unifidie.
19 Zab 22:6;Isa 53:3;Ebr 12:2 Wewe umejua kulaumiwa kwangu,
Na kuaibika na kufedheheka kwangu,
Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote.
20 Laumu imenivunja moyo,
Nami ninaugua sana.
Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna;
Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
21 Mt 27:34;Mt 27:48;Mk 15:36;Lk 23:36;Yn 19:28-29 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;
Na nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
22 Rum 11:9-10;2 Kor 3:14 Meza yao mbele yao na iwe mtego;
Naam, sikukuu zao sadaka ziwanase.
23 Macho yao yatiwe giza wasione,
Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
24 Uimwage ghadhabu yako juu yao,
Na ukali wa hasira yako uwapate.
25 Mdo 1:20 Makambi yao na yawe ukiwa,
Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.
26 Isa 53:4 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe,
Wanazidisha maumivu ya hao uliowatia jeraha.
27 Rum 9:31 Uwaongezee uovu juu ya uovu,
Wala wasipate msamaha kutoka kwako.
28 Kut 32:32;Eze 13:9;Lk 10:20;Flp 4:3;Ebr 12:23;Ufu 3:5;13:8;17:8 Na wafutwe katika kitabu cha uhai,
Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.
29 Nami niliye maskini na mtu wa huzuni,
Mungu, wokovu wako utaniinua.
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
31 Nayo yatampendeza BWANA kuliko ng’ombe,
Au ndama mwenye pembe na kwato.
32 Walioonewa watakapoona watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
33 Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafungwa wake.
34 Mbingu na nchi zimsifu,
Bahari na vyote viendavyo ndani yake.
35 Zab 57:1-3;102:13,16;Isa 14:32;44:26 Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda,
Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
36 Wazawa wa watumishi wake watairithi,
Nao walipendao jina lake watakaa humo.