Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi, wakati Doegi, Mwedomu alipomwendea Sauli na kumwambia, "Daudi ameingia nyumbani mwa Ahimeleki."
1 1 Sam 22:9-10;21:7 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?
Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 Zab 50:19;Mit 12:18;Zab 59:7 Ulimi wako watunga madhara,
Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.
3 Yer 9:4 Umependa mabaya kuliko mema,
Na uongo kuliko kusema kweli.
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu,
Ewe ulimi wenye hila.
5 Mit 2:22 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;
Atakuondolea mbali;
Atakunyakua hemani mwako;
Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6 Ayu 22:19;Zab 58:10 Nao wenye haki wataona;
Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7 Ayu 31:24,25;Zab 49:6 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,
Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake.
Aliutumainia wingi wa mali zake,
Na kufanya mali kimbilio lake.
8 Zab 92:13 Bali mimi ni kama mzeituni
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 Zab 54:6 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;
Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;
Mbele ya wacha Mungu wako.