Publicidade

Chamada

Por Bíblia Online

A chamada de Deus é irrevogável. Ele nos chamou das trevas para a sua maravilhosa luz — para sermos santos, discípulos e instrumentos de sua graça no mundo.

Chamados por Deus

Fostes chamados para a liberdade. A chamada de Deus é dom irrevogável que nos convida à santidade e ao serviço.

Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. Kwa maana imeandikwa: "Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu."

Mfano wa mateso ya Al-Masihi

Ninyi mliitwa kwa ajili ya haya, kwa sababu Al-Masihi naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo, ili mzifuate nyayo zake.

Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka.

ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema, bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Al-Masihi Isa tangu milele.

Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.

Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.

A resposta à chamada

Deus é fiel, pelo qual fostes chamados. Ele nos escolheu, nos capacitou e nos enviou com propósito eterno.

Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Isa Al-Masihi, Bwana wetu ni mwaminifu.

Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, ili mtu yeyote asijisifu mbele zake.

Tu zaidi ya washindi

Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wanaompenda, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake, ili kuwaletea mema.

Kwa kusudi hili Mungu aliwaita ninyi kupitia Injili tuliyowahubiria, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Petro akawajibu, "Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mungu.

Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.

Hukumu na wokovu

"Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

nilisema, Niko hapa, niko hapa.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-