Colheita
A colheita é princípio bíblico universal: colhemos o que semeamos. Quem semeia na fé e obediência colherá bênçãos abundantes do Senhor.
Semear e colher
Quem semeia no Espírito, do Espírito colherá vida eterna. Não nos cansemos de fazer o bem — ao tempo certo colheremos.
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoeshwa nayo matunda ya haki yenye amani.
Fidelidade na semeadura
Honra ao Senhor com as tuas primícias. O Senhor abrirá as janelas do céu e derramará bênção sem medida.
Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Mkizifuata amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya; ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa mavuno yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
Maana furaha imetoweka kwa wanadamu.
Imani na shangwe katika shida
Maana mtini hautachanua maua,
Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;
Taabu ya mzeituni itakuwa bure,
Na mashamba hayatatoa chakula;
Zizini hamtakuwa na kundi,
Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;
Walakini nitamfurahia BWANA
Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.