Publicidade

Consolo

Por Bíblia Online

O consolo de Deus é bálsamo para a alma ferida. Ele nos conforta em todas as tribulações para que possamos consolar outros com o mesmo consolo divino.

Deus consola

Ainda que eu ande pelo vale da sombra da morte, não temerei mal algum. O Senhor consola, guia e está sempre presente.

Hata nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

Sala ya kusifu
Zaburi ya Daudi.

Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:

Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,

sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini,

na kwa yule anayemtafuta;

Confiança na aflição

Eu sei que o meu Redentor vive. Deus é força e escudo — mesmo na tribulação, Ele nos sustenta e consola.

Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai,

naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.

Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,

bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;

Hakika Mungu ni wokovu wangu;

nitamtumaini wala sitaogopa.

Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu."

Mwenyezi Mungu mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,

"Mwenyezi Mungu ni msaada wangu; sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"

Heri wale wanaohuzunika,

maana hao watafarijiwa.

Lakini mimi, namtazama Mwenyezi Mungu kwa matumaini,

namngoja Mungu Mwokozi wangu;

Mungu wangu atanisikia mimi.

Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja kwenu.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-