Publicidade

Deus

Por Bíblia Online

Deus é a realidade suprema do universo — o criador, sustentador e redentor de tudo o que existe. Conhecê-lo é a essência da vida eterna e o maior privilégio da existência humana.

Quem é Deus

Não há santo como o Senhor. Tu és grande e fazes maravilhas — só tu és Deus. Sua majestade transcende toda compreensão.

"Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Mwenyezi Mungu,

hakuna mwingine zaidi yako;

hakuna Mwamba kama Mungu wetu.

"Tazama jinsi ulivyo mkuu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi! Hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe,

Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu.

Sifa kwa Mwenyezi Mungu

Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni Mungu wangu,

nitakutukuza na kulisifu jina lako,

kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu

umetenda mambo ya ajabu,

mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.

"Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,

wala njia zenu si njia zangu,"

asema Mwenyezi Mungu.

Deus é amor

Deus é amor. Quem permanece no amor permanece em Deus e Deus nele. Nós amamos porque Ele nos amou primeiro.

Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.

Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.

Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

Ikiwa mtu atasema, "Nampenda Mungu," lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemwona?

Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,

yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Buscar a Deus

Buscareis o Senhor e o encontrareis quando o buscardes de todo o coração. Provai e vede que o Senhor é bom.

Lakini kama mtamtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wote na kwa roho yote.

Onjeni mwone kwamba Mwenyezi Mungu ni mwema;

heri mtu yule anayemkimbilia.

Nilimwambia Mwenyezi Mungu, "Wewe ndiwe Bwana wangu;

pasipo wewe sina jambo jema."

Nani niliye naye mbinguni ila wewe?

Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.

Wakati ninaogopa,

nitakutumaini wewe.

Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,

uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.

Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima,

na kujipatia kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Viver com Deus

Sê forte e corajoso, porque o Senhor teu Deus é contigo. Em Deus encontramos a razão de existir.

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini!

Utukufu wa Sayuni

"Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja

na utukufu wa Mwenyezi Mungu umezuka juu yako.

Kwa maana Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

Jinyenyekezeni mbele za Mwenyezi Mungu, naye atawainua.

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-