Espírito
O espírito humano é a parte mais profunda do nosso ser — onde Deus habita, onde a fé se ancora e de onde brota a verdadeira adoração. A Bíblia nos chama a viver pelo Espírito.
A natureza do espírito
O espírito está pronto, mas a carne é fraca. A batalha entre carne e espírito é constante e exige vigilância.
Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu."
"Heri walio maskini wa roho,
maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.
Kwa hiyo nasema, nendeni kwa Roho wa Mungu, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Lakini tunda la Roho wa Mungu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.
Kwa kuwa tunaishi kwa Roho wa Mungu, basi, tuenende kwa Roho.
Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho wa Mungu ni uzima na amani.
O Espírito de Deus em nós
Vosso corpo é templo do Espírito Santo. Deus fortalece com poder no homem interior pelo seu Espírito.
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu wa Mungu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Lakini mtu aliyeungwa na Bwana Isa anakuwa roho moja naye.
Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho Mtakatifu wa Mungu.
Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia.
Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, ili Al-Masihi apate kukaa mioyoni mwenu kupitia kwa imani. Nami ninaomba kwamba mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo,
Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu tena, bali mlipokea Roho wa kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, "Abba, Baba." Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi tu watoto wa Mungu.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi tu watoto wa Mungu.
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu tena, bali mlipokea Roho wa kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, "Abba, Baba."
Lakini kama Al-Masihi anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu.
Vivyo hivyo, Roho wa Mungu hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa.
Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana Isa.
Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu.
Vida no Espírito
Deus é Espírito e importa que os que o adoram o adorem em espírito e em verdade. O Espírito vivifica e transforma.
Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii. Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana Isa, aliye Roho.
Wapendwa, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Isa Al-Masihi, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu.
Neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe pamoja na roho zenu. Amen.
Promessas do Espírito
Derramarei o meu Espírito sobre toda a carne. O Espírito revela, guia e capacita os filhos de Deus.
Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu
na kuwafahamisha maneno yangu.
Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,
bali makusudi hupimwa na Mwenyezi Mungu.
Kiburi hutangulia maangamizi,
roho ya majivuno hutangulia maanguko.
Ni afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu
miongoni mwa walioteswa
kuliko kugawana nyara na wenye kiburi.
Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,
mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
Taa ya Mwenyezi Mungu huchunguza roho ya mwanadamu,
huchunguza utu wake wa ndani.
Kisha akaniambia, "Hili ni neno la Mwenyezi Mungu kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho wangu Mtakatifu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu,
kwa sababu Mwenyezi Mungu amenipaka mafuta
kuwahubiria maskini habari njema.
Amenituma kuwafariji waliovunjika moyo,
kuwatangazia mateka uhuru wao,
na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao;
Nitawapa moyo usiogawanyika na kuweka roho mpya ndani yao; nitaondoa ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa hii mifupa: Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.
Cuidar do espírito
Cria em mim um coração puro e renova dentro de mim um espírito reto. O espírito quebrantado Deus não rejeita.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
Usinitupe kutoka mbele zako
wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
Unirudishie furaha ya wokovu wako,
unipe roho ya utii, ili initegemeze.
Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
moyo uliovunjika wenye toba,
ee Mungu, hutaudharau.
Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo,
na huwaokoa waliopondeka roho.
Usiweke tumaini lako kwa wakuu,
kwa wanadamu ambao hufa,
ambao hawawezi kuokoa.
Roho yao itokapo hurudi mavumbini,
siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Kama vile mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.
Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.
Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupatia sisi sehemu ya Roho wake Mtakatifu.
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wa Mungu wale wamwombao!"
Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
Lakini ni Roho iliyo ndani ya mwanadamu,
pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo ufahamu.
Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha,
au bakuli la dhahabu halijavunjika;
kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi,
au gurudumu kuvunjika kisimani,
nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka,
na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara za miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia.
Ishara zake ni kuu kama nini!
Na maajabu yake yana nguvu kama nini!
Ufalme wake ni ufalme wa milele;
enzi yake hudumu kizazi hadi kizazi.