Gratidão ao Senhor
A gratidão ao Senhor é resposta de amor diante da bondade divina. Louvar a Deus com cântico e magnificá-lo com ação de graças — isso é o que agrada ao Senhor.
Agradecer ao Senhor
Deus transformou nosso lamento em dança. Ele é digno de toda gratidão, em todo tempo e em toda circunstância.
Umegeuza msiba wangu kuwa ngoma;
Umeniondolea huzuni yangu, kunijalia furaha tele.
Ili nafsi yangu ikusifu,
Wala isinyamaze.
Ee BWANA, Mungu wangu,
Nitakushukuru milele.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Washangilie, wakufurahie,
Wote wakutafutao.
Waupendao wokovu wako
Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
Gratidão constante
Em tudo dai graças. Tudo o que Deus criou é bom, quando recebido com ação de graças e paz no coração.
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;
Nitaziondoa nadhiri zangu.
Wokovu hutoka kwa BWANA.