Pular para o conteúdo
Publicidade

Ler a Bíblia

Por Bíblia Online

Ler a Bíblia é essencial para a vida cristã. A Escritura é lâmpada para os pés, alimento para a alma e espada do Espírito. O cristão que lê a Bíblia é transformado pela Palavra.

A importância de ler

Meditar na Palavra dia e noite traz prosperidade e bom sucesso. Ler a Bíblia ilumina o entendimento e fortalece a fé.

Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.

Nuru katika Torati ya Mwenyezi Mungu

Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,

kunampa mjinga ufahamu.

Kuipenda Torati ya Mwenyezi Mungu

Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

Nina akili kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako.

Kutii Torati ya Mwenyezi Mungu

Kijana aisafishe njia yake jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

A Escritura é inspirada

Toda a Escritura é útil para ensinar, corrigir e instruir em justiça. Examine as Escrituras — nelas encontramos a vida eterna.

Maandiko yote yamevuviwa na Mungu, na yafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele. Maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi.

Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.

Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, hadi nitakapokuja.

Estudar com diligência

Os bereanos eram mais nobres porque examinavam as Escrituras diariamente. O estudo dedicado da Bíblia produz maturidade espiritual.

Hawa Waberoya walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.

Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika Torati ya Mwenyezi Mungu na kuwafundisha Waisraeli amri na sheria zake.

Walisoma kutoka kile Kitabu cha Torati ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.

Isa akawajibu, "Je, hampotei kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu?

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.

Faida za hekima

Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu

na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,

kutega sikio lako kwenye hekima

na kuweka moyo wako katika ufahamu,

na kama utaiita busara,

na kuita kwa sauti upate ufahamu,

na ukiitafuta kama fedha

na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,

ndipo utakapoelewa kumcha Mwenyezi Mungu

na kupata maarifa ya Mungu.

Kwa maana Mwenyezi Mungu hutoa hekima,

na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

Seja o primeiro